TAASISI YA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE YATEMBELEA BUNGE
Baadhi ya Viongozi wa Taasisi ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mkoni Pwani wakiwa kwenye Picha ya pamoja na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Pwani Subira Mgalu juzi walipotembelea Bunge kwa mualiko wa Mbunge huyo
Viongozi wa Taasisi ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mkoni Pwani wakiwa Bungeni wakifuatilia mijadala ya Bunge inayoendelea.
Na. Yohana Msafiri Kibaha, Pwani.
Taasisi ya kumbukumbu ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Mkoa wa Pwani imetembelea Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dodoma Februari 2, 2024 Kwa Mwaliko wa Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Pwani Bi. Subira Mgalu kwa lengo la kujifunza Shughuli za Bungeni.
Akizungumza na Mwàndishi wa habari hizi Katibu wa Taasisi hiyo Mkoani Pwani Omary Punzi amesema kuwa kitendo alichofanya Mbunge huyo kwa kuwakaribisha bungeni kimewapa faraja kubwa kwani wameweza kujifunza mambo mengi ambayo yanahusisha maslahi ya nchi.
"Kwa niaba ya Taasisi ya Mwalimu Nyerere nampongeza Mbunge Mheshimiwa Subira Mgalu kwa namna alivyotujali na tumepata uelewa kwa kujifunza"amesema
Pia alipongeza juhudi za Serikali ya awamu ya Sita ya Mh. Dk. Samia Suluhu Hassani kwa namna bunge lilivyokuwa linafanya kazi vizuri Kwa uchangamfu na kujibu hoja vizuri.
Mwisho
Comments
Post a Comment