BONANZA LA NYUMBU LAFANA, WACHEZAJI WAPYA WATAMBULISHWA KUIVAA AFRIKA LYON.


Wachezaji timu ya Nyumbu Fc wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kutambulishwa  katika bonanza lililofanyika kwenye viwanja vya Nyumbu Project


Na Gustafu Haule, Pwani.
 
BONANZA la michezo la kikosi cha Jeshi la Nyumbu lililopo Kibaha Mkoani Pwani limefanyika likienda sambamba na kutambulisha wachezaji wapya wa timu ya Nyumbu Fc.

Bonanza hilo limefanyika katika viwanja vya Nyumbu Project likihusisha mchezo wa mpira wa miguu ,mchezo wa kukimbiza Kuku pamoja na mchezo wa kuvuta kamba.

Washiriki wa mchezo wa kuvuta kamba uliofanyika jana katika bonanza la Nyumbu lililofanyika jana katika viwanja vya Nyumbu Project.


Aidha, katika mchezo wa mpira wa miguu bonanza hilo lilizishirikisha timu  ya Wanajeshi iliyocheza na timu ya Raia,timu ya Nyumbu Veterani iliyocheza na Nyika Veterani huku Bayi Veterani ikicheza na Kibaha Veterani.

Wachezaji wa timu ya Nyumbu Fc wakiwa pamoja na benchi lao la ufundi mara baada ya kutambulishwa katika bonanza la michezo lililofanyika  katika viwanja vya Nyumbu Project 


Katika mzunguko wa michezo hiyo timu mbili zilifanikiwa kutinga katika hatua ya fainali ikiwemo Nyumbu Veterani na Kibaha Veterani lakini hata hivyo Nyumbu Veterani aliibuka kuwa mshindi baada ya kuichapa Kibaha Veterani bao 1-0.

Mbali na michezo hiyo lakini pia katika bonanza hilo timu ya madaktari kutoka hospitali ya Rufaa Tumbi ilipiga Kambi  kwa ajili ya kuendesha zoezi la uchangiaji damu wa hiari zitakazosaidia wagonjwa pindi wanapokuwa na mahitaji.

Baadhi ya Wananchi waliojitokeza kuchangia damu kwa hiari katika bonanza la Nyumbu lililofanyika jana katika viwanja vya Nyumbu Project vilivyopo Kibaha Mkoani Pwani.


Kaimu Mkuu wa Kikosi cha Jeshi la Nyumbu Kanali Charles Kalambo, amesema kuwa Nyumbu imejipanga kuhakikisha wanafanya vizuri katika michezo.

Kalambo , amesema kuwa kwa sasa tayari wanayotimu ya Nyumbu Fc inayocheza ligi daraja la pili na kwamba kikosi kimejipanga kikamilifu kuhakikisha wanafanya vizuri kwakuwa wameweza kusajili wachezaji wazuri.

Kaimu Mkuu wa Kikosi cha Jeshi Nyumbu kilichopo Kibaha Mkoani Pwani Kanali Charles Kalambo akizungumza na wachezaji wa Nyumbu FC mara baada ya kumaliza bonanza lililofanyika jana katika viwanja vya Nyumbu Project.

Kalambo,ametumia nafasi hiyo kuwaomba wadau mbalimbali wa michezo kujitokeza katika kuisaidia timu hiyo ili iweze kufanya vizuri kwani matokeo mazuri ya timu hiyo ni fahari kwa Mkoa wa Pwani.

"Matumaini yetu ni kuona Nyumbu inapata matokeo mazuri lakini kikubwa ni kuomba sapoti kutoka ngazi za juu ikiwemo vyama vya michezo na wadau mbalimbali kwa kuwa timu ya Nyumbu Fc ndio timu pekee iliyofanikiwa kuingia katika mashindano ya ligi daraja la pili na endapo ikifanikiwa kuingia hatua nyingine itakuwa imetoa taswira ya Mkoa wa Pwani,"amesema Kalambo.

Kalambo,amesema Kikosi cha Nyumbu kitaendelea kuiunga mkono timu hiyo ambapo kwasasa tayari wametengeneza jezi na watakuwa wanazivaa katika siku mbili za wiki pamoja na kutoa hamasa mbalimbali lakini ili kufikia malengo wadau ni muhimu zaidi.

Mwenyekiti wa Nyumbu FC Jaffary Kilindo, amesema timu yake itaingia dimbani siku ya Jumatatu kucheza mzunguko wa pili wa ligi ya daraja la pili dhidi Afrika Lyon katika viwanja vya mabatini Mlandizi Kibaha .

Kilindo, amewahakikishia ushindi wanaPwani kwa kuwa kikosi chake ni kipana huku akishukuru wadau hususani Chama Cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA) kwa mchango wake mkubwa wa kuisaidia timu.

Afisa habari wa Nyumbu FC Mariam Songoro, amesema kuwa lengo la bonanza hilo ilikuwa ni kutambulisha usajili wa wachezaji wapya katika Kikosi hicho.

Songoro, amesema Kikosi kilichotangazwa katika bonanza hilo ni imara na kitakwenda kuleta ushindi mkubwa na hivyo kuipeleka timu katika mashindano mengine ya ngazi zinazofuata.

Songoro,amewataka mashabiki na wapenzi wa soka waliopo ndani na nje ya Mkoa wa Pwani kujitokeza kwa wingi siku ya Jumatatu kwa ajili ya kushuhudia jinsi ambavyo vijana wao wanavyolisakata kabumbu na hivyo kuondoka na ushindi mnene.

Hata hivyo,katika kuisaidia timu hiyo Kikosi cha Jeshi la Nyumbu siku ya jana waliendesha harambee iliyofanyika katika ukumbi wa Kambarage na kufanikiwa kupata kiasi cha Sh.milioni 5,842,000 ambapo kati ya hizo ahadi ni milioni 4,900,000 na pesa taslimu ni 942,000.

MWISHO 









Charles Kusaga - Club News Editor

Comments

Popular posts from this blog

RC PWANI AONGOZA WAKAZI PWANI KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA WAPIGA KURA

BARAZA LA MADIWANI KIBAHA MJINI LAMPONGEZA MKURUGENZI WAKE KWA KAZI NZURI ANAYOIFANYA SAMBAMBA NA KUONGEZA MAPATO.

RAIS SAMIA ATANGAZA KIBAHA MJINI KUWA MANISAPAA,MBUNGE KOKA AFURAHIA ASEMA KIBAHA ITANG'AA