Usingizi watajwa chanzo cha ajali Dodoma.
baadhi ya majeruhi wa ajali ya basi la kampuni ya Ally’s Star iliyotokea Januari 03,2024 eneo la mnada mpya Mkoani Dodoma wakiwa katika hospitali ya Rufa ya mkoa huo kwa matibabu mra baada ya kutokea ajali hiyo
Mwandishi wetu.
Dodoma. Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma limetaja chanzo cha ajali ya basi la kampuni ya Ally’s Star iliyotokea Januari 03,2024 eneo la mnada mpya Mkoani humo kuwa ni uchovu na usingizi wa dereva aliyekua akiendesha gari hilo
Kamanda wa Polisi Mkoani Dodoma Martin Otieno amesema changamoto hiyo imemsababishia dereva huyo ambaye bado hajafahamia jina kwa alikimbia mara baada ya ajali hiyo kushindwa kulidhibiti gari na kupelekea kupinduka.
Otieno amesema katika tukio hilo watu watano akiwemo mtoto mdogo minne nane walijeruhiwa na kupelekwa kupata matibabu katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Dodoma na kwamba kwa sasa hali zao zinaendelea vizuri.
Mmoja wa majeruhi ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha sita katika shule ya wavulana ya Kibiti Mkoani Pwani, Kulwa Lazaro amesema walianza safari saa 4 usiku kutoka Mkoani Shinyanga na walipoingia Jijini Dodoma ndipo walipopata ajali saa 12 asubuhi .
“Nilikuwa nimekaa mbele kwa dereva alikuwa anasinzia sijui ni kwa sababu ya uchovu? maana kuna muda tulikutana na gari dogo ambalo wengine tuliliona lakini yeye dereva aliliona ghafla na hivyo akalikwepa kwa kwenda upande wa pili wa barabara na baadaye alikaa sawa tukaendele na safari,” amesema Lazaro.
Amesema baada ya dereva kulikwepa hilo gari dogo waliendelea na safari lakini kutokana na usingizi alianza kutoka nje ya barabara na aliposhtuka alikuwa tayari ametoka kabisa na mbele yake kulikuwa na miti akawa anaikwepa asiigonge arudi barabarani.
“wakati huo wote hofu ilishatanda nikawa nasali huku naangalia na niliona dereva alipoona kuna miti mbele yake alianza kujitahidi ili asiigonge alitaka kurudi tena barabarani lakini katika harakati za kurudi barabarani ndipo gari lilimshinda na kupinduka.”
Amesema baada ya hapo kila mtu alikuwa anajiokoa maisha yake na wengine walianza kukanyagana ndani ya gari lakini yeye alitokea kwenye uwazi uliopo juu ya gari na abiria wengi walitoka kupitia uwazi huo.
Lazaro amesema yeye
alipata jeraha kichwani kwani gari lilipopinduka vioo vilimkata na wengine
wanne pia walipata majeraha madogo madogo ambapo wametibiwa na kuendelea na
safari yao.
“Hata hivyo tunamshukuru Mungu kwa kuwa hakuna aliyepoteza maisha kwenye hii ajali zaidi ya majeraha madogo ambayo tumeyapata, hata hivyo tumetibiwa na tutaendelea na safari yetu,” amesema Japhet
Comments
Post a Comment