Basi lapinduka likiwa safarini
Mwandishi wetu.
Dodoma. Abiria watatu wamejeruhiwa baada ya basi la kampuni ya Ally's waliokua wakisafiria kutoka Mkoani Shinyanga kwenda Dar es salaam kupinduka asubuhi ya leo katika eneo la Mnada mpya uliopo Mkoani Dodoma.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Martin Otieno amethibitisha kutokea ajali hiyo Januari 03, 2024 saa 12:15 asubuhi baada ya dereva wa basi hilo kushindwa kulithibiti na kupinduka.
" leo majira ya saa 12:15 asubuhi ndio hili tukio lilitokea na ajali hii imesababisha majeruhi watatu ambao majeraha yao ni ya kawaida na wanapatiwa matibabu hospitalini," amesema Otieno
Kamanda Otieno ametaja chanzo cha ajali ni dereva kushindwa kulithibiti kutokana na uchovu au matatizo ya kiafya hivyo kusababisha gari hilo kupinduka katika eneo hilo la mnada mpya jijini humo.
Ofisa habari wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma Jeneral, Renatha Mzanje ameongeza kuwa majeruhi hao wote hali zao zinaendelea vema na bado wanaendelea na matibabu .

Comments
Post a Comment