WANANCHI BAGAMOYO WALILIA BARABARA

Na. Sanjito Msafiri, Bagamoyo. Pwani
Wakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo Mkoani wameiomba Serikali kukamilisha ujenzi wa barabara ya TAMCO-MAPINGA inayojengwa kwa kiwango cha lami Ili kuwaondolea adha wanayokumbana nayo kwa sasa ikiwemo gharama kubwa ya nauli na kutumia muda mwingi barabrani.
Wameyasema hayo Desemba 01/2023 muda mfupi baada ya Halmashauri hiyo kuelezea utekelezaji wa ilani ya uchaguzi kwenye Mkutano uliofanyika Mjini Bagamoyo Mkoani Pwani ambao umehusisha watendaji wa ngazi mbalimbali,madiwani na viongozi wengine ukiongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Halina Okashi.

Baadhi ya watendaji wa ngazi mbalimbali wa Halmashauri ya Wilaya ya Bgamoyo katika Mkutano ulioleta taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi iliyobeba dhima ya miradi ya maendeleo kutoka kwa Mkuu wa wilaya hiyo Mh. Halima Okashi kwenye mkutano uliofanyika Mijni Bagamoyo
Kwa mujibu wa wakazi hao wamesema kero wanazokumbana nazo kwa sasa ni pamoja na kutumia muda mwingi barabrani kwa zaidi ya masaa mawili pamoja na gharama kubwa ya nauli ambayo ni sh 3500 kutoka Bagamoyo hadi Kibaha Loliondo hivyo ujenzi huo utawaondolea adha hiyo.
Mfanyabiashara wa samaki Katalina Samuel amesema kuwa uchakavu wa barabara ya Makofia Mlandizi unawapa kero kubwa ikiwemo uchovu kutokana na maumivu ya mtikisiko wa gari wakati wanasafiri kwani mashino ni mengi hivyo ni vema waharakishe ujenzi wa kiwango cha rami.
"Barabara ya Tamko mapinga ina umuhimu mkubwa sana kwa wananchi na kama itakamilika itarahisisha shughuli za Usafiri na usafirishaji ikilinganishwa na ilivyo sasa ukipanda kwenye daladala kuanzia Mailimoja hadi Bagamoyo unachelewa kufika na pia unakuwa umechoka na nauli ni kubwa kwakuwa gari linatumia muda mrefu njiani mesema Halima Salumu.
Kwa upande wake Mohamed Habibu ameishauri Halmashauri hiyo kuiboresha stendi ya Mabasi makubwa Ili kuwezesha mabasi hayo kuingia na kulipia ushuru kwani kutasaidia kuongeza mapato.
"Hata stendi ya mabasi ni vema ikaangaliwa Ili iwe imara na mabasi yote yawe yanaingia Ili kulipia ushuru wa huduma kwa kila basi moja hapo hata mapato yataongezeka tofauti na ilivyosasa mengine hayaingii"amesema Mohamed Habibu
Akijibu moja ya maswali yaliyoulizwa kwenye Mkutano huo lililolenga ujenzi wa barabara ya Makofia Mlandizi, na TAMCO-MAPINGA Mbunge wa Bagamoyo Mkoani Pwani Muharamí Mkenge amesema kuwa hivi sasa barabara hizo ziko kwenye hatua za mwisho Ili ujenzi wake kuanza na nyingine kuendelea.

"Kuhusu barabara ya Tamco Mapinga ujenzi wake utaendelea na tayari mikataba ilishasainiwa na hata ya Makofia Mlandizi imeshafanyiwa upembuzi yakinifu na muda si mrefu taratubu za ujenzi zitaanza"amesema
Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi mapema kwenye Mkutano huo ambao pia baadhi ya wananchi walipata nafasi ya kuhudhuria Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Halima Okashi amesema kuwa kiasi hicho zaidi ya sh.48 bilioni kimetekeleza miradi mbalimbali ikiwemo miundombinu ya barabara,elimu,afya na maji kwa Halmashauri zote mbili za Bagamoyo na Chalinze.
Amesema kuwa kwa mujibu wa tathmini waliyoifanya utekelezaji wa miradi hiyo mefikia lengo la asilimia 98 huku asilimia mbili zilizosalia wakitarajia kufikia ndani ya miezi sita ijayo nguvu kubwa ikielekezwa kwenye maeneo ya huduma zinazolenga jamii moja kwa moja.
"Tunataka kuhakikisha tunawaondokea wananchi wetu na hii ni dhamira kuu ya Serikali hivyo tutafikia asilimia 100 kama ambavyo tumejiwekea utaratibu"amesema
Akizungumzia kuhusu stendi ya mabasi
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bagamoyo Mohamed Usinga amesema kuwa wametenga eneo lenye ukubwa wa ekali 19 ambapo tayari wameshakamilisha andiko mradi ambapo utagahrimu zaidi ya sh 4.8 bilioni na itakuwa ya kisasa.
Mwisho
ReplyForward |
Comments
Post a Comment