WAFANYABIASHARA SOKO LA LOLIONDO KIBAHA WAPATA VIONGOZI WAPYA, MNEMBWE AENDELEA KUSHIKA USUKANI.





Na Gustafu Haule,Pwani

 

WAFANYABIASHARA wa Soko la Mnarani lililopo Loliondo Kata ya Tangini katika Halmashauri ya Mji Kibaha wamefanikiwa kupata viongozi wapya watakaoongoza Soko hilo kwa kipindi  cha miaka mitatu ijayo.


Viongozi hao wamepatikana kufuatia uchaguzi uliofanyika Disemba 22 mwaka huu sokoni hapo ambapo hatahivyo nafasi ya mwenyekiti imekwenda kwa Mohamed Omari (Mnembwe).

 

Mwenyekiti wa Soko la Mnarani Ndugu Mohamed Omari (Mnembwe)

Mnembwe,ambaye alikuwa anatetea nafasi yake ameshinda kwa kishindo baada ya kumbwaga mpinzani wake Anthony Maganga ambaye alijikuta anapata kura 130 dhidi ya Mnembwe aliyepata kura 423.

 


Pichani wapiga kura wakipiga kura kuchagua viongozi katika Soko hilo

Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo msimamizi wa uchaguzi kutoka ofisi ya Mtendaji Kata ya Tangini Idd Hassan,amesema kuwa Mnembwe ameshinda nafasi hiyo baada ya kupata kura nyingi zaidi ya mwenzake .

 

"Nafasi ya mwenyekiti ilikuwa na wagombea wawili akiwemo Levis Anthony Maganga na Mohamed Said Omari (Mnembwe) lakini katika uchaguzi Maganga amepata kura 130 na Mnembwe amepata kura 423 hivyo Kwa mamlaka niliyopewa namtangaza Mnembwe kuwa mwenyekiti wa Soko hili,"anasema Hassan.

 

Aidha kwa mujibu wa Hassan nafasi nyingine zilizowaniwa katika uchaguzi huo ni pamoja na nafasi ya Katibu wa Soko iliyochukuliwa na Sheiza Steven aliyepata kura 302 na kumshinda Abdul Kombo(211) pamoja na Emmanuel Mwasha(106) huku nafasi ya Katibu msaidizi imekwenda kwa Leonard Msimbe(548).

 


Pichani shughuli za uchaguzi wa Viongozi ukiendelea katika Soko hilo

Pia,nafasi ya mwekahazina ilikuwa na wagombea wawili akiwemo Josephu John na Lazaro Josephu ambapo hata hivyo Josephu John ameibuka kuwa mshindi baada ya kupata kura 434 dhidi ya mpinzani wake aliyepata kura 263.

 

Aidha nafasi nyingine zilizowaniwa katika uchaguzi huo ni uongozi wa kitengo cha Mabucha ambapo mwenyekiti ni Saimon Chirwa(29) na katibu ni Tunda Tajiri(25),wakati kitengo cha Ndizi Mbivu ni Venance Mkumbo(26) na katibu ni Lazaro Stephano(17) huku Mjumbe ni Gasper Msimbe.

 

Kitengo cha Malimbichi walioshinda ni Salim Mdimu aliyechukua nafasi ya uenyekiti (17) wakati Katibu ni Hssan Konda(36) huku kitengo cha Mamalishe mwenyekiti ni Mwanahamis Mohamed (09) na katibu ni Grace Shilla huku Mjumbe ni Abdallah Hamisi(62).

 

Upande wa Matunda mwenyekiti ni Khatibu Omari(50) na katibu ni Amina Mwinyimvua (45) huku Mjumbe ni Amos Selemani wakati upande wa Fremu viongozi wake ni Paul Mashimba(37) na katibu wake Swedi Mkumba  (38).

 

Kitengo cha nafaka aliyeshinda nafasi ya mwenyekiti ni Ally Mfinanga (46) na Katibu wake ni Juma Soke(47) huku Mjumbe ni Josephu Mushi (47) na upande wa Bodaboda aliyeshinda kuwa mwenyekiti ni Zuberi Bakari(14).

 

Katika upande wa Kuku mwenyekiti ni Bakari Msuya na kitengo cha Nyanya mwenyekiti ni Greyson Richard(37) na Katibu ni Sheba Kalage(40) huku Mjumbe ni Idd Nassoro (40) wakati upande wa stendi mwenyekiti ni Lazaro Benjamin (106) na Katibu wake ni Yusuf Mmari(123) na Mjumbe ni Zawadi Mbonde(123).

 

Hata hivyo,upande wa bidhaa mchanganyiko Mwiru Ngombale ameibuka kuwa mshindi wa nafasi ya mwenyekiti kwa kupata kura 120 wakati Thadeo Paskali ameshinda nafasi ya Katibu Kwa kupata kura 57 na kuwabwaga wapinzani wake Eliana Massawe(39) huku Zuberi Mazwazwa akiambulia kura 25.

 

Akizungumza mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi Mnembwe amesema kuwa amefurahi kutangazwa kuwa mshindi lakini ushindi wake umetokana na kazi nzuri iliyofanyika kipindi cha nyuma cha uongozi wake.

                                      

Mnembwe,amesema kuwa baada ya ushindi wake wafanyabiashara wategemee mazuri zaidi hasa katika kutatua changamoto zinazowakabili ikiwemo kujenga paa eneo la Matunda,kufanya marekebisho eneo la bidhaa mchanganyiko na mchele pamoja na maeneo mengine.


Mwisho 




Club News Editor - Charles Kusaga

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

RC PWANI AONGOZA WAKAZI PWANI KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA WAPIGA KURA

BARAZA LA MADIWANI KIBAHA MJINI LAMPONGEZA MKURUGENZI WAKE KWA KAZI NZURI ANAYOIFANYA SAMBAMBA NA KUONGEZA MAPATO.

RAIS SAMIA ATANGAZA KIBAHA MJINI KUWA MANISAPAA,MBUNGE KOKA AFURAHIA ASEMA KIBAHA ITANG'AA