RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN ATOA MAELEKEZO KUHUSIANA NA JANGA LA MAFURIKO YALIYOTOKEA HANANG - MANYARA



Na Gustafu Haule

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan , ametoa maelekezo kuhusu namna ya kugharamia mazishi ya watu waliofariki kufuata mafuriko yaliyotokea Wilayani Hanang Mkoani Manyara.

Rais Samia,amemuelekeza Waziri Mkuu  Kassim Majaliwa kuwa Serikali igharamie mazishi ya wote waliopoteza maisha kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa zilizonyesha Wilayani humo.

Rais Samia ,ametoa maelekezo hayo leo Desemba 04,2023 huku akiwa na masikitiko makubwa ya kuwapoteza wananchi wake.

Amesema,majeruhi wote wapatiwe matibabu yote yanayostahili kwa gharama za Serikali huku Vyombo vya Ulinzi na Usalama vikiendelea kutoa Msaada wa dharura na Uokoaji.

 Amemtaka, Mkuu wa Kitengo cha Maafa cha Ofisi ya Waziri Mkuu kuhakikisha Wananchi wote ambao Makazi yao yamesombwa na maji wapate makazi ya muda kwaajili ya kuwasitiri Wananchi hao.

 Aidha Rais Samia ametaka tathimini ya kina ifanyike juu ya maafa hayo na vitengo na taasisi zote za Serikali zinazohusika kuwepo eneo la tukio na kufanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha hali inarejea kawaida.

MWISHO


Club News Editor

Comments

Popular posts from this blog

BARAZA LA MADIWANI KIBAHA MJINI LAMPONGEZA MKURUGENZI WAKE KWA KAZI NZURI ANAYOIFANYA SAMBAMBA NA KUONGEZA MAPATO.

RAIS SAMIA ATANGAZA KIBAHA MJINI KUWA MANISAPAA,MBUNGE KOKA AFURAHIA ASEMA KIBAHA ITANG'AA

RC PWANI AFURAHISHWA NA UTENDAJI KAZI WA MKURUGENZI WA KIBAHA MJINI DKT.ROGERS SHEMWELEKWA