MATUMIZI YA GESI YAZINGATIWE KUJIHADHARI NA MAJANGA YA MOTO
Na.
Mwandishi wetu , Pwani
Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Pwani Jenifa
Shirima amewasihi Wananchi hasa wanawake kuzingatia matumizi bora ya nishati
safi ya Gesi kwani kufanya hivyo kutasaidia kujihadhari dhidi ya majanga ya
moto. Amewataka wananchi kuhakikisha wanatoa taarifa mapema pindi yanapotokea
majanga ya moto.
Amesema kuwa
matumizi ya gesi ni moja ya vyanzo vya moto endapo haitatumika kwa usahihi.
Amewasihi kinamama kuhakikisha wanapotumia mitungi ya gesi wanakuwa wanaifunga
kwa usahihi baada ya kuitumia na kuiweka sehemu salama ambayo watoto hawawezi
kuifikia na kisha kufungua na gesi kuvuja na kusababisha majanga hayo ya moto.
hayo wakati wa Tamasha la Bibi Titi Mohammed, 2023 lililofanyika kwenye uwanja wa Ujamaa, Ikwirir Rufiji Mkoa wa Pwani.




Comments
Post a Comment