MAONYESHO SHUGHULI ZA KLABU ZA WAANDISHI WA HABARI!!!!
Umoja wa Klabu za Waandishi wa habari Tanzania kupitia wanachama wake 28 ambao ni klabu za Wandishi wa Habari za mikoa umefanya maonyesho ya shughuli mbalimbali za Klabu jijini Dodoma yalipo makao makuu ya Umoja huo.
Shughuli mbalimbali ziliizoonyeshwa na klabu ni zile za kiuandishi habari zinazoleta mabadiliko kwenye jamii na shughuli za kiuchumi zinazoinua kipato cha wanahabari na Klabu kwa ujumla.




Katika maonyesho hayo pia klabu hizi za waandishi wa habari zilionyesha utambuzi wa michango mbalimbali ya waandishi wa habari kwenye jamii kwa kupewa tuzo na wadau mbalimbali waliotambua michango hiyo.
Maonyesho haya yalileta washiriki kufahamu shughuli mbalimbali na hatua mbalimbali za Klabu katika kutekeleza majukumu yao na mafanikio yao kutoka hatua moja kwenda hatua nyingine bora zaidi.
Comments
Post a Comment