MAJALIWA AHITIMISHA TAMASHA LA BIBI TITI MOHAMED WILAYANI RUFIJI MKOANI PWANI
Na Gustafu Haule,Rufiji Pwani.
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amempongeza waziri wa Tamisemi na Mbunge wa Jimbo la Rufiji Mohamed Mchengerwa kwa kazi kubwa aliyoifanya katika kipindi kifupi cha utekelezaji wa ilani katika Sekta ya Miundombinu.
Ameyasema hayo katika
kilele cha Miaka miwili ya kumbukizi ya Hayati Bibi Titi Mohamed Mwanasiasa Mwanamke
wa kwanza Tanganyika kushiriki waziwazi katika juhudi za kupigania uhuru
wa Tanganyika kipindi cha ukoloni.
Amesema hatua ya Jimbo
la Rufiji kuwa na madaraja ya uhakika ni hatua nzuri hasa kwa mikoa ya kusini
kuendeka bila changamoto yeyote.
Pia ametoa salamu za
Rais Dkt.Samia suluhu Hassan zenye lengo la kuendelea kumkumbuka na
kumuenzi Bibi Titi Mohamed kwa kuthamini mchango wake katika harakati za
uhuru wa Tanganyika.
Amesema kauli mbiu
ambayo italeta tija ya kumkumbuka Bibi Titi Mohamed wakati wa sasa na
baadaye ni kudumisha umoja, uzalendo na kuacha ujumbe kwa vizazi vijavyo.
Waziri Majaliwa,
amemuelezea Bibi Titi kuwa ni mwanamke jasiri, mkakamavu, na kujitoa kwake
katika kuleta usawa wa kijinsia kwa wanawake na wanaume.
Amesema kuendelea
kumuenzi Bibi Titi ni kuendeleza usawa wa kijinsia kwa wanawake, na mchango
wake katika kuleta maendeleo kuwa ni shujaa, uhuru tulionao ni juhudi za
Mashujaa waliopita.
Ameeleza kuwa mawazo
ya Bibi Titi ni mfano wa kuigwa kwa viongozi wanawake kama anavyofanya
Rais Samia.
Ameendelea kusema,
kuwa maadhimisho hayo yawe chachu kupinga ukatili wa kijinsia na wanawake
washiriki katika siasa na kufanya vizuri katika kuleta matokea chanya.
Amesema Taifa lina
kila sababu ya kukumbuka kazi nzuri na nguvu za Rais Dkt.Samia kung'aa
kimataifa kwa kuwa mwanadiplomasia namba moja kuimarisha uchumi, fursa za
kibiashara, utalii na mageuzi makubwa ya uchumi.
Amesema Rais
Samia ameendelea kusimamia fursa za uchumi, elimu na diplomasia, siasa safi na
ustaarabu.
Aidha ameimarisha
sekta binafsi na kuendeleza mifumo ya sheria, na kuwezesha sekta binafsi
kufanya kazi vizuri na kuhimiza ulipaji kodi.
Aisha,Majaliwa
amesema kwa kipindi kifupi Dkt. Samia ameendelea kuhimiza utoaji wa elimu bure,
kuongeza mikopo, maboresho mitaala ya elimu ili vijana wajiajiri, sekta ya afya
hospital mpya 107 , huduma za kibingwa hadi ngazi za halmashauri.
Amesema
Rais Samia amehimarisha huduma za matibabu ya Moyo, ini, mifupa na uroto hii
yote ni kuhakikisha anarudisha huduma ya afya karibu na wananchi.
Waziri Mkuu amesema
katika upande wa Siasa nafasi ya Mwanamke inazidi kuonekana kwa uwiano wa
nafasi za teuzi kwa wanawake.
MWISHO.
Comments
Post a Comment