LIGI YA MABINGWA AFRICA YAENDELEA





Na Gustafu Haule

 

 LIGI ya Mabingwa barani Afrika imeendelea leo Desemba 2, ambapo Klabu ya Yanga Sc imejikuta ikiambulia sare ya kufungana  1-1 na mabingwa watetezi, Al Ahly katika mchezo wa Kundi D uliochezwa  Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

 

Kipindi cha kwanza timu zote mbili hakuna aliyeweza kuchungulia lango la mwenzake lakini kipindi cha pili kilianza kwa kila mmoja kutumia mbinu mbadala ikiwemo kufanya mabadiliko ya wachezaji wake.

 

Mabadiliko hayo yalizaa matunda ambapo Mabingwa watetezi Al Ahly walipata bao dakika ya 86 kupitia Percy Tau ambapo Yanga waliweza kisawazisha mnamo dakika ya 90+1  kupitia  kiungo  mahiri kutoka Ivory Coast, PacĂ´me Zouzoua.

 


Kwa Matokeo hayo Al Ahly imefikisha pointi nne na kuendelea kuongoza Kundi D kwa pointi moja zaidi ya wote, CR Belouizdad ya Algeria na Medeama ya Ghana, wakati Yanga yenye pointi moja inashika mkia baada ya mechi mbili.

 

Mechi inayofuata Yanga SC itasafiri hadi nchini Ghana kucheza na Medeam  Ijumaa ya Desemba 8, wakati Al Ahly watawakaribisha CR Belouizdad Jijini Cairo.

 

MWISHO

 

















Club News Editor

Comments

Popular posts from this blog

BARAZA LA MADIWANI KIBAHA MJINI LAMPONGEZA MKURUGENZI WAKE KWA KAZI NZURI ANAYOIFANYA SAMBAMBA NA KUONGEZA MAPATO.

RAIS SAMIA ATANGAZA KIBAHA MJINI KUWA MANISAPAA,MBUNGE KOKA AFURAHIA ASEMA KIBAHA ITANG'AA

RC PWANI AFURAHISHWA NA UTENDAJI KAZI WA MKURUGENZI WA KIBAHA MJINI DKT.ROGERS SHEMWELEKWA