Uadilifu wa jamii na Malezi ya Vijana na Watoto karne ya 21

 













NA JULIETH MKIRERI,  KIBAHA

 

KUNA usemi unasema samaki mkunje angali mbichi, ikimaanisha kwamba mtoto anatakiwa kufundishwa vitu vingi ikiwemo maadili akiwa bado mdogo.

 

Mtoto akifundishwa jambo akiwa bado mdogo ni rahisi kulishika na kulifanyia kazi  lakini pia atakuwa na kumbukumbu kila anapoona anaenda tofauti na kukumbuka alichofundishwa.

 

Zamani kulikua na utaratibu wa bibi kuwasimulia wajukuu hadithi ambazo kwa namna moja au nyingine zilikuwa na mafundisho ambayo yaliishi kwa watoto na walikuwa wakiyafuata tofauti na siku hizi.

 

Karne hii ya 21 iko na mabadiliko makubwa watoto wanajikita kuangalia katuni na tamthilia zinavyoonyeshwa kwenye TV.

 

Tofauti na ilivyo zamani bibi kutenga muda wa kusimulia hadithi wajukuu zake kwasasa bibi wanakaa kwenye seble za nyumbani kwao wakiwa na wajukuu wanafuatilia tamthilia kwa pamoja.

 

Kutokana na mabadiliko hayo vipo vitu vingi vimebadilika kulingana na teknolojia na hii sasa inawataka wazazi kubadilisha mfumo wa malezi.

 

Annastazia Rugaba ni Meneja Utetezi kutoka Twaweza ambaye anawakumbusha wazazi kuendana na mabadiliko ya kiteknolojia na kuachana na malezi ya kizamani kuwanusuru watoto.

 

Akiwa katika Jukwaa la Ufahamu wa Kiraia linaloandaliwa na Shirikaa Vijana la Youth Partnership Countrywide (YPC) anasema malezi ya karne ya 21 yanatakiwa kuwa na mabadiliko.

 

Anasema wazazi na walezi wanatakiwa  kuwalea watoto kulingana na mna teknolojia ilivyobadilika ili kuwalinda na mabadiliko ya kimaadili.

 

Anasema Teknolojia inavyozidi kukua inatakiwa kuendana na malezi ya watoto katika karne ya 21 ili kuwaepusha kujiingiza kwenye mambo ambayo hayaendani na Maadili ya Kiafrika.

 

Anasema mitandao ya kijamii pia imekuwa sababu ya mabadiliko kwa watoto wengi na hata kuiga mambo ambayo ni kinyume na maadilili ya kiafrika.

 

Anasema kutokana na hali hiyo watoto wanatakiwa kulelewa na kufundishwa njia sahihi wakiwa bado wadogo wakue katika njia sahihi.

 

Vile vile wazazi wanatakiwa kuwa waangalifu kwa vijana wao kwa kuwafuatilia kwenye matumizi ya simu, tv pamoja na baadhi ya vinywaji ambavyo wakati mwingine vinaongezewa vitu vinavyowabadilisha mfumo kwenye miili yao.

 

Rugaba alisema “Malezi ya karne ya 21 ni shida isiyoelezeka kwenye mabadiliko ya kiteknolojia yanaenda kasi isivyo kawaidawazazi wanatakiwa waachane na kuwalea watoto kizamani wabadilike kulingana na nyakati ili kuwaepusha na kwenda kinyume na maadili” .

 

 Alisema kutokana na mabadiliko yaliyopo sasa uaminifu katika Taasisi ya ndoa umepungua kutokana na ongezeko la migogoro  ya ndoa jambo ambalo limekuwa likisababisha watoto kulelewa na mzazi mmoja.

 

“Takwimuambazo zimechukuliwa kwenye madawati ya Jinsia baada ya watu kwenda kuripoti zinaonyesha kwamba kila saa moja ndoa 13 zina migogoro talaka zinaongezeka kwa kasi”.

 

"Taasisi ya ndoa awali ilikuwa inaaminika kuwa msingi mzuri wa  kulea watoto lakini kwasasa tunalalamikia, na hao baadhi ya viongozi ambao tunawalalamikia kwasasa wametoka kwenye familia gani na vijana vibaka wanatoka wapi, hao wote ni kwenye ndoa ambazo nyingi zimeingia migogoro na watoto wanalelewa humo ama kuachwa wenyewe” alieleza Rugaba.

 

Anabainisha kwamba zamani kulikuwa na changamoto kwenye malezi lakini hazikuwa nyingi kama ilivyo sasa, mabadiliko hayo pia sambamba na migogoro ni sababu inayochangia siku hizi mabinti wengi kupata watoto na hawataki wanaume ni kwakuona taasisi ya ndoa haina haja tena .

 

“Mahusiano ya jinsia moja pia yameongezeka tunakokwenda hali inazidi kuwa mbaya dawa za p2 wanatumia mabinti kuzuia mimba kitu ambacho wataalamu wa afya wanasema usitumie zaidi ya mara mbili kwa mwaka na sasa wanauziana kama pipi jambo ambalo baadae inakuwa na athari kubwa kwa watoto bila wao kujua” analeza.

 

Mwenyekiti wa Bodi ya YPC Martine Mng’ong’o anasema kwasasa ni vizuri wazazi wakabadilika kwenye malezi ya vijana wao ili baadae wasije wakaenda kinyume na maadili kwani kwasasa  wengi wanajifunza mambo mengi kupitia teknolojia tofauti na ilivyokuwa zamani.

 

Mng’ong’o anasema YPC iligundua kuwepo kwa mabadiliko kwa vijana  kupitia teknolijia jambo ambalo limewasukuma kutoa elimu hiyo kwa vijana na wazazi kupitia Jukwaa hilo ambalo linalofanyika kila mwisho wa mwezi.

 

Naye Mwalimu  Amina Kijuu kutoka shule ya Msingi Kambarage iliyopo Kibaha anasisitiza mabadiliko ya malezi kwa wazazi ili kuwanusuru vijana kufanya vitu ambavyo ni tofauti na maadili yao.

 

Kijuu anaeleza kwamba hali ya maadili kwa watoto imebadilika tofauti na ilivyokuwa zamani ambapo amesisitiza wazazi kuwalea watoto kiimani jambo ambalo litakuwa msaada kusimamia imani zao.

 

" Tuwasisitize watoto kushi kwenye imani zao, tuwakazanie kushiriki ibada na kufuata mafundisho ya kiimani na hii itawasaidia kuwa na hofu ya Mungu" anasema.

 

Mwalimu huyo pia anaeleza kwamba endapo wazazi watasimama kwenye nafasi zao na kuwa karibu na watoto itapilunguza vitendo vya ukatili ikiwemo ubakaji na ulawiti kwa watoto ambao kwasasa umeshamiri kwenye maeneo mbalimbali.

 

Mwisho.

Comments

Popular posts from this blog

BARAZA LA MADIWANI KIBAHA MJINI LAMPONGEZA MKURUGENZI WAKE KWA KAZI NZURI ANAYOIFANYA SAMBAMBA NA KUONGEZA MAPATO.

RAIS SAMIA ATANGAZA KIBAHA MJINI KUWA MANISAPAA,MBUNGE KOKA AFURAHIA ASEMA KIBAHA ITANG'AA

RC PWANI AFURAHISHWA NA UTENDAJI KAZI WA MKURUGENZI WA KIBAHA MJINI DKT.ROGERS SHEMWELEKWA