Elimu ya tembo inavyoboresha maisha ya wanafunzi .
Beatrice Lihaku ni mwalimu wa somo la mahusiano kati ya Tembo na wanafunzi shuleni Na Julieth Ngarabali. Hana wasiwasi tena wa kutimiza ndoto yake ya kuelimika na kuwa kiongozi mwenye mafanikio katika jamii. Uhakika huu umetokana na kikwazo cha kwenda shule kusoma kuondo lewa. Huyu ni Joseph Sefu, mwanafunzi Shule ya Msingi Mlimani iliyopo Kata ya MangĂșla ‘B’ Halmashauri ya Mji wa Ifakara mkoani Morogoro. Joseph Sefu, mwanafunzi Shule ya Msingi Mlimani akieleza namna yeye na familia yake walivyonufaika na somo laTembo shuleni. Wanafunzi wa shule tatu za msingi na awali za Mlimani, Kanyenja na Magombera akiwemo Joseph walikuwa wanakabiliwa na changamoto ya tembo kuvamia makazi ya watu katika Kata ya Mang’ula ‘B’.hivyo muda mwingi wakawa ni wenye hofu tu. Tembo hawa walikuwa wakifanya uharibifu wa makazi, mashamba, kujeruhi na hata kuondoa uhai wa watu matukio yaliyochangia hofu na wasiwasi mkubwa kwa watoto wakiwemo wale wa chini ya miaka nane. Hali hii iliwawek...