Posts

Showing posts from December, 2023

WAFANYABIASHARA SOKO LA LOLIONDO KIBAHA WAPATA VIONGOZI WAPYA, MNEMBWE AENDELEA KUSHIKA USUKANI.

Image
Na Gustafu Haule,Pwani   WAFANYABIASHARA wa Soko la Mnarani lililopo Loliondo Kata ya Tangini katika Halmashauri ya Mji Kibaha wamefanikiwa kupata viongozi wapya watakaoongoza Soko hilo kwa kipindi  cha miaka mitatu ijayo. Viongozi hao wamepatikana kufuatia uchaguzi uliofanyika Disemba 22 mwaka huu sokoni hapo ambapo hatahivyo nafasi ya mwenyekiti imekwenda kwa Mohamed Omari (Mnembwe).   Mwenyekiti wa Soko la Mnarani Ndugu  Mohamed Omari (Mnembwe) Mnembwe,ambaye alikuwa anatetea nafasi yake ameshinda kwa kishindo baada ya kumbwaga mpinzani wake Anthony Maganga ambaye alijikuta anapata kura 130 dhidi ya Mnembwe aliyepata kura 423.   Pichani wapiga kura wakipiga kura kuchagua viongozi katika Soko hilo Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo msimamizi wa uchaguzi kutoka ofisi ya Mtendaji Kata ya Tangini Idd Hassan,amesema kuwa Mnembwe ameshinda nafasi hiyo baada ya kupata kura nyingi zaidi ya mwenzake .   "Nafasi ya mwenyekiti ilikuwa na wago...

KIBAHA YAZINDUA PROGRAM YA MALEZI, MAKUZI NA MAENDELEO YA AWALI YA MTOTO

Image
  Julieth Ngarabali,   Kibaha Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha imezindua program Jumuishi ya Taifa ya malezi ,makuzi na maendeleo ya awali ya Mtoto ( PJT MMMAM) kwa lengo la  kukabiliana na tatizo la udumavu, kuwapa huduma bora za malezi ya awali na programu za elimu ambazo zitawawezesha  watoto wenye umri wa miaka 0 hadi 8 kukua na kufikia ukuaji timilifu na hatimaye kuwa watu wazima wenye uwezo wa kufanya kazi za uzalishaji mali kwa tija hivyo kuchangia ukuaji wa uchumi wa Tanzania pamoja na kujenga jamii yenye amani na utulivu.   Uzinduzi huo umefanyika kwa kushirikisha wadau mbalimbali ikiwemo taasisi ya Anjita Child Development Foundation,viongozi wa dini, kisiasa,sekta binafsi, wataalam mbali mbali na wamiliki wa vituo vya kulelea watoto wadogo katika halmashauri hiyo. Program hii inaongozwa na kauli mbiu,"mtoto kwanza na watoto wetu tunu yetu"" A kizungumza kwenye uzinduzi huo kaimu Mkurugenzi halmashauri ya Kibaha ,Fatuma Kisalazo amesema ...

ANUSURIKA KUUAWA MARA TATU PORI LA AKIBA KILOMBERO.

Image
  Ally Libenanga aliyewahi kunusurika kuuawa mara tatu na mamba na viboko wakati akivua samaki katika bwawa la Ndolo  Na Gustaph Haule, Kilombero ILIKUWA Novemba 23 Saa 10:30 jioni naingia katika kambi ya wavuvi ya Isherero katika Kijiji cha Idui kilichopo jirani na pori la akiba la Kilombero lililopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba Mkoani Morogoro.  Safari hiyo ya saa ,9 iliyoanzia katika eneo la Mikumi hadi katika Kijiji hicho ilinikutanisha na Ally Athumani Libenanga (43) aliyewahi kuwa mvuvi haramu katika bwawa la Ndolo lililopo katika pori hilo.  Libenanga, baba wa watoto wanne kwa sasa ameachana na shughuli ya uvuvi haramu baada ya kukumbwa na mikasa mbalimbali ikiwemo kushambuliwa na Kiboko na Mamba ambayo imekuwa ikitishia uhai wake. “Uvuvi haramu ni sumu,” anasema Libenanga akiwa nje ya nyumba yake ya chumba kimoja iliyojengwa kwa kutumia miti na udongo na kisha kuezekwa na nyasi . Pichani baadhi ya nyumba za Wavuvi katika kambi ya Isherero iliyopo ji...

KYEM GENERAL SUPPLIES YAPIGA JEKI UJENZI CCM

Image
Na Gustafu Haule,Pwani CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Tangini iliyopo Kibaha Mjini imepokea msaada wa vifaa vya ujenzi  kutoka kampuni ya uuzaji wa chuma chakavu na usambazaji wa vifaa vya ujenzi Kyem General Supplies vyenye thamani zaidi ya Sh. milioni 3.5. Kyem ,imetoa vifaa hivyo kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa ofisi ya CCM ya Kata hiyo katika  hatua ya kukamilisha msingi ambapo vifaa walivyotoa ni nondo 40,kokoto,mchanga ,mbao na misumari. Msaada huo umekabidhiwa leo Disemba 21 na  Mkurugenzi Msaidizi wa kampuni ya Kyem General Supplies Martha Jackson kwa Katibu wa CCM Kata ya Tangini Sophia Mtase hafla ambayo imefanyika katika eneo la ujenzi wa ofisi hiyo iliyopo eneo la Loliondo. Akizungumza mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo Martha amesema kuwa kampuni yake ilipata maombi ya kusaidia ujenzi huo kupitia mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Tangini Shauri Yombayomba ambapo baada ya kupokea ombi hilo kampuni ilikaa na kujadili jambo hilo na hivyo kufikia maamuzi ya k...

UHIFADHI POR LA AKIBA KILOMBERO UTAKAVYOLIOKOA BWAWA LA MWALIMU NYERERE

Image
Ngiri wakiwa katika moja ya hifadhi Mkoani Morogoro Na Julieth Mkireri, Kilombero. WAKATI Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anapandisha hadhi pori tengefu la Kilombero na kuwa pori la akiba huenda wengi hawakujua eneo hilo ni muhimu kwa kiasi gani katika kuimarisha upatikanaji wa uhakika wa umeme hapa nchini. Pori  tengefu la Kilombero, lililoanzishwa mwaka 1952 wakati wa ukoloni, lilipandishwa hadhi kuwa pori la akiba Februari mwaka huu na Rais Samia, hatua iliyoongeza ulinzi na uhifadhi katika eneo hilo muhimu nchini.  Pori la Akiba la Kilombero ni miongoni mwa maeneo muhimu katika uendelevu wa bwawa la kufua umeme la Mwalimu Nyerere kwa kuwa linachangia takriban theluthi mbili ya maji. Kwa mujibu wa Rais Samia, Mto Ruaha Mkuu unachangia asilimia 15 ya maji huku Mto Luega ukichangia asilimia 19 na asilimia 65 zilizobaki ni kutoka Mto Kilombero na vyanzo vyake vingine vya maji. Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Gissima Nyamo-Hanga elieleza Septemba mwaka ...