SHULE YA MSINGI MKOANI YADAI WAZAZI ZAIDI YA SH.MILIONI 168,
Na Gustaphu Haule,Pwani SHULE ya Msingi mkoani yenye mchepuo wa kiingereza iliyopo kata ya Tumbi katika Manispaa ya Kibaha Mkoani Pwani ipo katika wakati mgumu wa kutekeleza majukumu yake kutokana na baadhi ya wazazi kushindwa kulipa ada kwa wakati. Shule hiyo ya serikali ilianzishwa mwaka 2018 ili kuwawezesha wanafunzi kupata masomo sawa na Shule za Kiingereza za binafsi ( Private) lakini changamoto iliyopo hivi sasa ni wazazi kushindwa kulipa ada ambayo ni Sh.400,000 kwa mwaka. Ada hiyo ni mgawanyo wa mihula miwili ambapo kila baada ya miezi Sita mzazi anatakiwa kulipa Sh.200,000 lakini bado wazazi wanashindwa kulipa jambo ambalo linapelekea uendeshaji wa Shule hiyo kuwa mgumu. Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Adelhelma Chawa akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake juzi amesema kuwa mpaka kufikia Julai 11,2025 shule hiyo inawadai Wazazi kiasi cha Sh.milioni 168,956,000. Mkuu wa Shule ya Msingi Mkoani iliyopo katika Manispaa ya Kibaha Adelhelma Chawa akizungumza na...