RC PWANI ATAKA MRADI WA IPOSA UTOE MATOKEO CHANYA KWA VIJANA

Na Gustaphu Haule, Pwani MKUU wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge, ameielekeza Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima kuhakikisha programu ya Mpango wa IPOSA inakuwa na matokeo chanya kwa kuwajengea vijana uwezo wa kujiajiri na kuajirika. IPOSA ni Mpango ulioandaliwa na Taasisi ya Elimu ya Watu wazima wa elimu changamani kwa Vijana walio nje ya Shule. Kunenge ametoa maelekezo hayo wakati akifunga mafunzo ya walimu wa programu hiyo yaliyofanyika Oktoba 2,2025 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha. Mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge akizungumza na wasimamizi wa mradi wa IPOSA katika mkutano uliofanyika Oktoba 2,2025 katika ukumbi mdogo wa Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha. Alisema kuwa elimu inayotolewa kupitia IPOSA haipaswi kubaki kwenye vyeti pekee, bali iwe chachu ya mabadiliko katika maisha ya vijana ambao wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya ajira. “Mradi huu wa IPOSA lazima uwe na matokeo ya kweli, vijana wanapaswa kufundish...